Dua ya Nabii Yunus Wakati wa Shida (Dhun-Noon)
لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنَ الظَّالِمِينَ.
Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, kutakasika ni Kwako; hakika mimi nilikuwa miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao.
Dua sahihi na adhkar zilizothibitishwa kutoka katika Qur'an na mafundisho ya Mtume Muhammad ﷺ. Hifadhi ya moyo, amani ya nafsi, na kinga ya muumini katika kila nyakati za maisha.
لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنَ الظَّالِمِينَ.
Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, kutakasika ni Kwako; hakika mimi nilikuwa miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao.
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْهَمِّ وَالْحَزَنِ، وَالْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَالْبُخْلِ وَالْجُبْنِ، وَضَلَعِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ.
Ee Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga Kwako kutokana na hamu na huzuni, na kutoweza na uvivu, na ubakhili na uoga, na kuelemewa na madeni na kudhulumiwa au...
حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ.
Mwenyezi Mungu anatutosha, Naye ndiye Msimamizi bora zaidi.
لاَ بَأْسَ، طَهُورٌ إِنْ شَاءَ اللَّهُ.
Hapana neno, ni kutakasika (kwa madhambi) Mwenyezi Mungu akipenda.
بِسْمِ اللَّهِ (mara 3)، أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ (mara 7).
Kwa jina la Mwenyezi Mungu (mara 3). Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na kwa uwezo Wake kutokana na shari ya ninachokihisi na ninachokiogopa (mara 7).
أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ.
Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyetupwa mbali na rehema Yake.
اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلاَلِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ.
Ewe Mwenyezi Mungu, nitosheleze kwa vilivyo halali Vyako nisihitaji vilivyo haramu Vyako, na unitajirishe kwa fadhila Zako nisiwe na haja na yeyote asiyekuwa We...
اللَّهُمَّ لاَ سَهْلَ إِلاَّ مَا جَعَلْتَهُ سَهْلاً، وَأَنْتَ تَجْعَلُ الْحَزْنَ إِذَا شِئْتَ سَهْلاً.
Ewe Mwenyezi Mungu, hakuna jambo rahisi ila lile Ulilolifanya Wewe kuwa rahisi, na Wewe unalifanya jambo gumu kuwa jepesi Ukitaka.
إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي، وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika sisi Kwake tutarejea. Ewe Mwenyezi Mungu, nilipe ujira katika msiba wangu huu, na unibadilishie kitu kilicho bora za...
اللَّهُمَّ إِنَّا نَجْعَلُكَ فِي نُحُورِهِمْ، وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شُرُورِهِمْ.
Ewe Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakuweka Wewe mbele ya shingo zao (ili Ututosheleze nao), na tunajikinga Kwako kutokana na shari zao.
يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغِيثُ، أَصْلِحْ لِي شَأْنِي كُلَّهُ، وَلاَ تَكِلْنِي إِلَى نَفْسِي طَرْفَةَ عَيْنٍ.
Ewe Uliye Hai daima, Ewe Msimamia kila kitu, kwa rehema Yako ninaomba msaada; nitengenezee mambo yangu yote, wala usiniachie nafsi yangu mwenyewe hata kwa kiasi...
أُعِيذُكَ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّةِ، مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ وَهَامَّةٍ، وَمِنْ كُلِّ عَيْنٍ لاَمَّةٍ.
Ninakukinga kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyokamilika, kutokana na kila shetani na kila mdudu mwenye sumu, na kutokana na kila jicho baya lenye kudhuru.