Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuache Wadda, wala Suwa'u wala Yaghuth na Yauq na Nasr" Amesema Ibn Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Haya ni majina ya watu wema katika watu wa Nuhu.
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عن ابن عباس رضي الله عنهما في قول الله تعالى : (وَقَالُوا لا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلا سُوَاعًا وَلا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا) قال: "هذه أسماء رجال صالحين من قوم نوح، فلما هَلَكوا أَوحى الشَّيطان إلى قَومِهِم أنِ انْصِبُوا إلى مَجَالِسِهِم الَّتي كانوا يَجْلِسون فيها أنصَابًا، وسَمُّوها بأسمَائِهِم، فَفَعَلُوا، ولم تُعْبَد، حتَّى إِذَا هَلَك أُولئك ونُسِيَ العلم عُبِدت".
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Ibn Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao-Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuache Wadd, wala Suwa'u wala Yaghuth na Yauq na Nasr" Akasema: "Haya ni majina ya watu wema katika watu wa Nuhu, walipokufa shetani aliwajulisha watu wao kuwa wekeni katika vikao vyao ambavyo walikuwa wakikaa hapo masanamu, na yaiteni kwa majina yao, wakafanya hivyo, na hayakuabudiwa, mpaka walipokufa hao na elimu ikasahaulika yakaabudiwa".
English translation
Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him) reported in explanation of Allah's statement: {And said: Never leave your gods and never leave Wadd or Suwā‘ or Yaghūth and Ya‘ūq and Nasr} [Sūrat Nūh: 23]. These are names of some pious men of the people of Nūh. When they died, Satan inspired their people to prepare and place idols at the places where they used to sit and to call those idols after their names. The people did so, but the idols were not worshiped till those people (who built them) had died and the original purpose for the existence (of those idols) had been forgotten
Maelezo
Ana tafsiri Ibn Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Aya hii tukufu kuwa miungu hii ambayo ameitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu- Kuwa watu wa Nuhu waliusiana kuendelea kuiabudu baada ya kuwa amewakataza Nabii wao Nuhu ziwe juu yake sala na salamu- kutomshirikisha Mwenyezi Mungu- kuwa majina hayo asili yake ni majina ya watu wema miongoni mwao, walichupa mipaka ndani yake kwa ushawishi wa Ibilisi kwao mpaka wakatundika picha zao, Basi jambo likakuwa katika picha hizi mpaka yakawa masanamu yanaabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu.
Faida
- Nikuwa kuchupa mipaka kwa watu wema ni sababu ya kuwabudu kinyume na Mwenyezi Mungu na kuiacha dini moja kwa moja.
- Tahadhari ya kupiga picha na kutundika picha, hasa hasa picha za waheshimiwa.
- Tahadhari kutokana na vitimbi vya shetani na kuileta kwake batili katika sura ya haki.
- Tahadhari kutokana na uzushi na mambo ya kuzua hata kama lengo la mfanyaji litakuwa zuri.
- Nikuwa kupiga picha ni katika nyenzo zinazopelekea katika shirki, hivyo ni lazima kutahadhari kupiga picha za viumbe vyenye roho.
- Kujua thamani ya uwepo wa elimu na madhara ya kukosekana kwake.
- Nikuwa sababu ya kukosekana kwa elimu ni kufa wanachuoni.
- Kutahadhari na kuiga, nakuwa hilo linaweza kumpelekea mfanyaji wake katika kutoka katika Uislamu.
- Kutangulia shirki katika umma zilizotangulia.
- Nikuwa majina haya matano yaliyotajwa ni katika viabudiwa vya watu wa Nuhu.
- Kubainishwa kubebana na kusaidiana watu wa batili juu ya batili yao.
- Kufaa kuwaombea mabaya makafiri kwa njia ya ujumla.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.