Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 5645

Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْرًا يُصِبْ مِنْهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo.

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "If Allah wills good for someone, He makes him suffer from afflictions."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehama na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu akitaka kheri kwa yeyote katika waja wake waumini huwapa mtihani katika nafsi zao na mali zao, na familia zao, kwa kile kinachotokea kwa muumini ikiwemo kurejea kwa Allah Mtukufu kwa maombi na dua, na kufutiwa makosa, na kunyanyuliwa daraja.

Faida

  • Nikuwa muumini anakabiliwa na mabalaa mbali mbali.
  • Mtihani unaweza kuwa alama ya mapenzi ya Allah kwa mja wake, ili amnyanyue daraja yake, na ampandishe cheo chake, na amfutie madhambi yake.
  • Himizo la kuwa na subira wakati wa matatizo na kutolalama.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)