Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 4497

Atakayekufa hali yakuwa anaomba kinyume na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, ataingia motoni

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قال: قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم كَلِمَةً وَقُلْتُ أُخْرَى، قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: «مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللهِ نِدًّا دَخَلَ النَّارَ» وَقُلْتُ أَنَا: مَنْ مَاتَ وَهُوَ لَا يَدْعُو لِلهِ نِدًّا دَخَلَ الْجَنَّةَ.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- neno moja nami nikasema neno jingine, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekufa hali yakuwa anaomba kinyume na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, ataingia motoni" Na mimi nikasema: Atakayekufa hali yakuwa haombi mungu mwingine ataingia peponi.

English translation

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: "The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said something and I said another thing. The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: 'Whoever dies while invoking besides Allah another equal will enter Hellfire.' And I say: 'Whoever dies while not invoking besides Allah another equal will enter Paradise.'"

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeelekeza chochote katika vile ambavyo vinapasa kuwa vya Mwenyezi Mungu pekee kwa asiyekuwa yeye, kama kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutaka msaada kwa asiyekuwa yeye, na akafa katika hali hiyo basi huyu ni katika watu wa motoni. Na akaongeza bin Masuod radhi za Allah ziwe juu yake kuwa atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika pepo.

Faida

  • Ibada hazielekezwi ila kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee.
  • Ubora wa tauhidi, nakuwa atakayekufa katika tauhidi ataingia peponi, hata kama ataadhibiwa kwa baadhi ya madhambi yake.
  • Hatari ya ushirikina, nakuwa atakayekufa katika ushirikina ataingia motoni.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)