Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. HE-64632

Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamrisha achukue miongoni mwa ng'ombe katika kila thelathini ndama alianza kufuatana na ng'ombe wengine, wa kiume au kike

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ مُعَاذٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا وَجَّهَهُ إِلَى الْيَمَنِ أَمَرَهُ أَنْ يَأْخُذَ مِنَ الْبَقَرِ مِنْ كُلِّ ثَلَاثِينَ تَبِيعًا أَوْ تَبِيعَةً، وَمِنْ كُلِّ أَرْبَعِينَ مُسِنَّةً، وَمِنْ كُلِّ حَالِمٍ -يَعْنِي مُحْتَلِمًا- دِينَارًا أَوْ عَدْلَهُ مِنَ المَعَافِرِ، ثِيَابٌ تَكُونُ بِالْيَمَنِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Muadhi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamrisha achukue miongoni mwa ng'ombe katika kila thelathini ndama alianza kufuatana na ng'ombe wengine, wa kiume au kike, na katika kila arobaini mwenye miaka miwili, na kutoka kwa kila anayeishi humo asiye muislamu Dinari au kitu chenye thamani sawa na Dinari kama Maafiri, nazo ni nguo hutengenezwa Yemen.

English translation

Mu‘ādh (may Allah be pleased with him) reported: When the Prophet (ﷺ) sent him to Yemen, he instructed him to take as Zakah on cattle; one Tabī‘ (a one-year-old male calf) or Tabī‘ah (a one-year-old female calf) for every thirty, and one Musinnah (a two-year-old cow) for every forty. He also commanded that from every adult—meaning one who has reached puberty—a dinar or its equivalent in garments from Ma‘āfir, a type of clothes produced in Yemen, be taken.

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yake kwenda Yemen kwa ajili ya kuwafundisha watu na kuwafikishia ujumbe, na miongoni mwa yale aliyomuamrisha achukue kutoka kwa Waislamu zaka za ng'ombe zao katika kila ng'ombe thelathini achukue dume moja au ng'ombe aliyeanza kufuatana na wengine machungani; naye ni yule aliyetimiza mwaka moja, na katika kila ng'ombe arobaini achukue ng'ombe mkamilifu; naye ni yule aliyetimiza miaka miwili. Na achukue jizia (kodi) kutoka kwa watu wa kitabu, Mayahudi na Wakristo, kwa kila mwanaume aliyebalehe, Dinari, au kinacholingana na Dinari katika nguo za Yemen ziitwazo: Maafari.

Faida

  • Jizia haichukuliwi isipokuwa kwa yule aliyebalehe; kwa sababu kigezo cha mtu asiyechukuliwa kodi ni: Ni yule ambaye haitakiwi kumuua akitekwa: Kama mtoto mdogo, na mwanamke, na wengineo.
  • Jizia makadirio yake yanarudi katika jitihada za kiongozi, kwa sababu zinatofautiana kulingana na kutofautiana kwa maeneo na zama, na utajiri na ufakiri, na ushahidi juu ya hilo nikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndiye aliyetoa makadirio hayo kwa watu wa Yemen, akasema kumwambia Muadhi: "Chukua kwa kila aliyebalehe Dinari", wakati huo huo jizia iliongezeka katika makadirio ya Omari radhi za Allah ziwe juu yake wakati alipoweka kiwango kwa watu wa Sham.l
  • Kutilia umuhimu ukusanyaji wa zaka, na kumuwakilisha mwenye kukusanya ni katika majukumu ya kiongozi.
  • Tabii: Ni yule aliyetimiza mwaka mmoja, na akaingia mwaka wa pili, na ameitwa tabii; kwa sababu bado anamfuata mama yake.
  • Dinari: Ni pesa ya dhahabu, na Dinari ya kislamu: Uzito wake ni gramu nne na robo ya dhahabu (4.25gm).

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)