Nyuma

Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamrisha achukue miongoni mwa ng'ombe katika kila thelathini ndama alianza kufuatana na ng'ombe wengine, wa kiume au kike

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ مُعَاذٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا وَجَّهَهُ إِلَى الْيَمَنِ أَمَرَهُ أَنْ يَأْخُذَ مِنَ الْبَقَرِ مِنْ كُلِّ ثَلَاثِينَ تَبِيعًا أَوْ تَبِيعَةً، وَمِنْ كُلِّ أَرْبَعِينَ مُسِنَّةً، وَمِنْ كُلِّ حَالِمٍ -يَعْنِي مُحْتَلِمًا- دِينَارًا أَوْ عَدْلَهُ مِنَ المَعَافِرِ، ثِيَابٌ تَكُونُ بِالْيَمَنِ.

Kutoka kwa Muadhi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamrisha achukue miongoni mwa ng'ombe katika kila thelathini ndama alianza kufuatana na ng'ombe wengine, wa kiume au kike, na katika kila arobaini mwenye miaka miwili, na kutoka kwa kila anayeishi humo asiye muislamu Dinari au kitu chenye thamani sawa na Dinari kama Maafiri, nazo ni nguo hutengenezwa Yemen.

Mu‘ādh (may Allah be pleased with him) reported: When the Prophet (ﷺ) sent him to Yemen, he instructed him to take as Zakah on cattle; one Tabī‘ (a one-year-old male calf) or Tabī‘ah (a one-year-old female calf) for every thirty, and one Musinnah (a two-year-old cow) for every forty. He also commanded that from every adult—meaning one who has reached puberty—a dinar or its equivalent in garments from Ma‘āfir, a type of clothes produced in Yemen, be taken.

Jizia haichukuliwi isipokuwa kwa yule aliyebalehe; kwa sababu kigezo cha mtu asiyechukuliwa kodi ni: Ni yule ambaye haitakiwi kumuua akitekwa: Kama mtoto mdogo, na mwanamke, na wengineo.

Jizia makadirio yake yanarudi katika jitihada za kiongozi, kwa sababu zinatofautiana kulingana na kutofautiana kwa maeneo na zama, na utajiri na ufakiri, na ushahidi juu ya hilo nikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndiye aliyetoa makadirio hayo kwa watu wa Yemen, akasema kumwambia Muadhi: "Chukua kwa kila aliyebalehe Dinari", wakati huo huo jizia iliongezeka katika makadirio ya Omari radhi za Allah ziwe juu yake wakati alipoweka kiwango kwa watu wa Sham.l

Kutilia umuhimu ukusanyaji wa zaka, na kumuwakilisha mwenye kukusanya ni katika majukumu ya kiongozi.

Tabii: Ni yule aliyetimiza mwaka mmoja, na akaingia mwaka wa pili, na ameitwa tabii; kwa sababu bado anamfuata mama yake.

Dinari: Ni pesa ya dhahabu, na Dinari ya kislamu: Uzito wake ni gramu nne na robo ya dhahabu (4.25gm).

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Jami' at-Tirmidhiy · Hadith Na. HE-64632 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali · Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
tirmidhi:he:64632