Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 1336

Amemlaani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- mtoa rushwa na mpokea rushwa katika hukumu

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: لَعَنَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الرَّاشِيَ وَالْمُرْتَشِيَ فِي الْحُكْمِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: "Amemlaani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- mtoa rushwa na mpokea rushwa katika hukumu".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) cursed the one who gives a bribe and the one who receives a bribe to influence a judgment.

Maelezo

Aliomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mtoa rushwa na mchukuaji wake na mpokeaji wake. Na miongoni mwake ni kile kinachotolewa kwa mahakimu ili wapindishe hukumu wanayoisimamia; ili mtoaji aitumie kama njia ya kufikia lengo lake pasina haki.

Faida

  • Ni haramu kutoa rushwa, na kuichukua, na kuwa wakala wake, na kusaidia; kwa sababu ndani yake kuna kusaidizana katika batili.
  • Rushwa ni katika madhambi makubwa; kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kamlaani mpokeaji wake na mtoaji wake.
  • Rushwa katika mlango wa kesi na hukumu ni dhulma kubwa na ni dhambi kubwa mno; kwani hapa kuna dhulma na kuhukumu kwa yale ambayo hakuyateremsha Mwenyezi Mungu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)