Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Ibn Majah · Na. HE-4716

Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ بُسْرٍ رضي الله عنه أَنَّ رَجُلاً قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ إِنَّ شَرَائِعَ الإِسْلاَمِ قَدْ كَثُرَتْ عَلَيَّ، فَأَخْبِرْنِي بِشَيْءٍ أَتَشَبَّثُ بِهِ، قَالَ: «لاَ يَزَالُ لِسَانُكَ رَطْبًا مِنْ ذِكْرِ اللَّهِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdallah bin Busri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sheria za Uislamu zimekuwa nyingi kwangu, hebu nieleze kitu ambacho nitashikamana nacho, akasema: "Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu".

English translation

‘Abdullah ibn Busr (may Allah be pleased with him) reported that a man said: O Messenger of Allah, the legislations of Islam have become too much for me, so inform me of something to hold on to. He said: "Keep your tongue moist with the remembrance of Allah."

Maelezo

Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ibada za sunna zimekuwa nyingi kwake mpaka zikamshinda kwa sababu ya udhaifu wake, kisha akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali nyepesi itakayompa thawabu nyingi atakayoshikamana nayo na adumu nayo. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuelekeza kuwa ulimi wake uwe mbichi utikisike kwa kudumu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kila wakati na kila hali; kama kumsabihi na kumhimidi na kumtaka msamaha na kumuomba na mfano wake.

Faida

  • Fadhila za kudumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu ni kufanya sababu za kupata malipo kuwa nyepesi.
  • Watu kuzidiana katika mafungu yao katika milango ya wema na kheri.
  • Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa ulimi, kwa kumsabihi na kumhimidi, na kukiri kuwa hapana mola muabudiwa wa haki ila yeye, na kumtukuza, na mengineyo pamoja na moyo kwenda sambamba na ulimi, hili linakaa nafasi ya ibada nyingi za sunna.
  • Kuchunga kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya muulizaji kwa kumjibu kila linalomfaa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)