Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Ibn Majah · Na. HE-4307

Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي العَبَّاسِ سَهْلِ بْنِ سَعِدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ، فَقَالَ: «ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النَّاسُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abul Abbasi Sahli bin Sa'di As-saai'diy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nijulishe amali ambayo nikiifanya atanipenda Mwenyezi Mungu na watu watanipenda, akasema: "Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda".

English translation

Abu al-‘Abbās Sahl ibn Sa‘d as-Sā‘idi (may Allah be pleased with him) reported: A man came to the Prophet (ﷺ) and said: O Messenger of Allah, guide me to a deed which, if I do it, Allah will love me and people will love me. He said: "Be indifferent to worldly life; Allah will love you, and be indifferent to what people have; people will love you."

Maelezo

Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali ambayo akiifanya Mwenyezi Mungu atampenda na watu watampenda, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Atakupenda Mwenyezi Mungu utakapoacha yasiyo na msingi katika Dunia, na yale yasiyokunufaisha katika Akhera, na ukaacha yale yanayoweza kuwa na madhara katika dini yako, na watu watakupenda utakapoyapa nyongo yaliyoko mikononi mwao miongoni mwa vitu vya kidunia; kwa sababu wanayapenda kulingana na tabia zao za asili, na atakayebanana nao katika hayo watamchukia, na atakayewaachia watampenda.

Faida

  • Ubora wa kuipa nyongo dunia, nayo: Ni mtu kuacha yasiyofaa katika Akhera.
  • Kuipa nyongo dunia daraja yake ni kubwa kuliko unyenyekevu; kwa sababu unyenyekevu ni kuacha mambo ambayo huenda yakakudhuru, na kuipa nyongo dunia ni kuacha yasiyofaa katika Akhera.
  • Amesema Assanadi: Hakika Dunia inapendeka kwa watu, yeyote atakayepambana nao humo atachukiza kwao kwa kadiri ya hilo, na atakayewaacha na hicho wanachokipenda atapendeka ndani ya nyoyo zao kwa kiwango cha hilo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)