Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Ibn Majah · Na. HE-4721

Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: إنه سمع نبي الله صلى الله عليه وسلم يقول: «لَو أَنَّكُمْ تَتَوَكَّلُونَ عَلَى اللهِ حَقَّ تَوَكُّلِهِ، لَرَزَقَكُمْ كَمَا يَرْزُقُ الطَّيْرَ، تَغْدُو خِمَاصًا وَتَرُوحُ بِطَانًا».

Tafsiri ya Kiswahili

imepokewa Kutoka kwa Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba".

English translation

‘Umar ibn al-Khattāb (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Prophet of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "If only you rely upon Allah the way you should, He will provide for you as He provides for birds: They set out hungry in the morning and return with full bellies in the evening."

Maelezo

Anatuhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuzuia madhara katika mambo ya Dunia na Akhera, kwani hakuna yeyote mwenye kutoa wala kunyima wala kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Yeye Aliyetakasika na Kutukuka, Na tufanye sababu zinazoleta manufaa na kuzuia madhara, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa dhati, wakati wowote tutakapofanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaotoka asubuhi wakiwa na njaa, kisha wanarudi jioni matumbo yakiwa yamejaa, na kitendo hiki kwa ndege ni aina ya kufanya sababu za kutafuta riziki, bila kubweteka wala uvivu.

Faida

  • Ubora wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, nakuwa ni katika sababu kubwa ambazo huvuta riziki.
  • Kumtegemea Mwenyezi Mungu hakupingani na kufanya sababu, kwani kaeleza kuwa kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa uhakika hakupingani na kutoka asubuhi na kurudi jioni katika kutafuta riziki.
  • Sheria kutilia umuhimu matendo ya moyo; kwa sababu kutegemea ni katika matendo ya moyo.
  • Kutegemea sababu pekee ni mapungufu katika dini, na kuacha kufanya sababu ni mapungufu ya akili.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)