عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ أَهْلُ الْكِتَابِ يَقْرَؤُونَ التَّوْرَاةَ بِالْعِبْرَانِيَّةِ، وَيُفَسِّرُونَهَا بِالْعَرَبِيَّةِ لِأَهْلِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تُصَدِّقُوا أَهْلَ الْكِتَابِ وَلَا تُكَذِّبُوهُمْ، وَقُولُوا: {آمَنَّا بِاللهِ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْنَا} [البقرة: 136] الْآيَةَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuwa Mayahudi na Manaswara wakiisoma Taurati kwa lugha ya Kiebrania, na kutafsiria Waislamu kwa lugha ya Kiarabu, basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala ni waongo, na semeni hivi {Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yote yaliyoteremshwa kwetu sisi} (Al-Baqara:36).
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The People of the Book used to read the Torah in Hebrew and expound on it in Arabic to the Muslims. So, the Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Neither believe nor disbelieve the People of the Book but say: {We believe in Allah and what has been sent down to us.} [Surat al-Baqarah: 136]."
Waliyoyaeleza Mayahudi na Manaswara, yapo katika sehemu tatu: Sehemu ya kwanza inakwenda sawa na Qur'ani na Sunna hivyo sehemu hii inakubaliwa. Sehemu ya pili: Inatofautiana na Qur'ani na Sunna, sehemu hii ni batili hufanywa kuwa ni ya uongo. Sehemu ya tatu: Hakuna kwenye Qur'ani wala Sunna habari inayohusu ukweli wake au uongo wake, basi habari kama hii haifanywi kuwa ya kweli au ya uongo.