Nyuma

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ زِيَادِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه قَالَ: ذَكَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْئًا، فَقَالَ: «ذَاكَ عِنْدَ أَوَانِ ذَهَابِ الْعِلْمِ» قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَكَيْفَ يَذْهَبُ الْعِلْمُ، وَنَحْنُ نَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَنُقْرِئُهُ أَبْنَاءَنَا وَيُقْرِئُهُ أَبْنَاؤُنَا أَبْنَاءَهُمْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ؟ قَالَ: «ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ زِيَادُ، إِنْ كُنْتُ لَأُرَاكَ مِنْ أَفْقَهِ رَجُلٍ بِالْمَدِينَةِ، أَوَلَيْسَ هَذِهِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى يَقْرَؤونَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ، لَا يَعْمَلُونَ بِشَيْءٍ مِمَّا فِيهِمَا؟!».

Imepokelewa kutoka kwa Ziyaad Bin Labiid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu" Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni vipi inaondoka elimu, na hali yakuwa sisi tunaisoma Qur'ani na tunawasomesha watoto wetu na watoto wetu wanawasomesha watoto wao mpaka siku ya Kiyama? Akasema: "Akukose mama yako ewe Ziadi ikiwa nitakuzingatia wewe ni miongoni mwa wajuzi katika mji wa Madina, hivi hawa siyo Mayahudi na Manaswara wanaisoma Taurati na Injili, na hawafanyii kazi chochote katika yale yaliyomo?!"

Ziyād ibn Labīd (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) mentioned something and said: "That will be at the time when knowledge disappears." I said: "O Messenger of Allah, how will knowledge disappear when we recite the Qur’an and teach it to our children, and they teach it to their children (and so on) until the Day of Judgment?" He said: "May your mother be bereaved of you, O Ziyād! I thought you were the most knowledgeable man in Madīnah. Is it not the case with these Jews and Christians who read the Torah and the Gospel, yet they do not act upon anything therein?!"

Kuwepo kwa Misahafu na vitabu kwenye mikono ya watu, haviwafai pasina kuvifanyia kazi.

Kuondoshwa elimu kunakuwa kwa mambo mengi, miongoni mwayo ni: Kufariki kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kufa kwa Maulamaa, na kuacha kuifanyia kazi elimu.

Miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondoka elimu na kuacha kuifanyia kazi.

Kuhimizwa kuifanyia kazi elimu, na hayo ndiyo makusudio.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. HE-65045 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Ni sahihi kwa sababu ya hadithi nyinginezo · Imepokelewa na Ibnu Maajah
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:65045