Dua ya Qur'ani: Kuomba Kukubaliwa Amali Njema
رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Mola wetu Mlezi! Tutakabalie (amali yetu); hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Dua sahihi na adhkar zilizothibitishwa kutoka katika Qur'an na mafundisho ya Mtume Muhammad ﷺ. Hifadhi ya moyo, amani ya nafsi, na kinga ya muumini katika kila nyakati za maisha.
رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Mola wetu Mlezi! Tutakabalie (amali yetu); hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ
Mola wetu Mlezi! Tujaalie tuwe wanyenyekevu Kwako, na katika vizazi vyetu ujaalie umma unaonyenyekea Kwako, na utuonyeshe ibada zetu na utukubalie toba yetu; ha...
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
Mola wetu Mlezi! Tupe duniani mema, na Akhera mema, na utukinge na adhabu ya Moto.
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
Mola wetu Mlezi! Tummulie subira, na uimarishe nyayo zetu, na utusaidie tushinde watu makafiri.
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
Mola wetu Mlezi! Usituchukulie hatia tukisahau au tukikosea.
رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا
Mola wetu Mlezi! Usitutwike mzigo mzito kama ulivyowatwika wale waliokuwa kabla yetu.
رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
Mola wetu Mlezi! Usitutwike tusiyoyaweza; na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu; Wewe ndiye Mlinzi wetu, basi tusaidie tushinde watu makafiri.
رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ
Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema kutoka Kwako; hakika Wewe ndiye Mpaji mkuu.
رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ
Mola wetu Mlezi! Wewe hakika ndiwe Mkusanyaji wa watu kwa Siku isiyo na shaka; hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi.
رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na utukinge na adhabu ya Moto.
رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ
Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyoyateremsha, na tumemfuata Mtume huyu, basi tuandike miongoni mwa wanaoshuhudia.
رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu, na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na uimarishe nyayo zetu, na utusaidie tushinde watu makafiri.