Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 12%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

kuzidishachochoteradhi

Sahih Muslim · Na. HE-1751

Hukumu za Swala na Tohara

عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ: تُوُفِّيَتْ إِحْدَى بَنَاتِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «اغْسِلْنَهَا ثَلاَثًا، أَوْ خَمْسًا أَوْ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ، إِنْ رَأَيْتُنَّ بِمَاءٍ وَسِدْرٍ، وَاجْعَلْنَ فِي الآخِرَةِ كَافُورًا -أَوْ شَيْئًا مِنْ كَافُورٍ-، فَإِذَا فَرَغْتُنَّ فَآذِنَّنِي»، قَالَتْ: فَلَمَّا فَرَغْنَا آذَنَّاهُ، فَأَلْقَى إِلَيْنَا حِقْوَهُ، فَقَالَ: «أَشْعِرْنَهَا إِيَّاهُ»، وَقَالَتْ: وَجَعَلْنَا رَأْسَهَا ثَلاَثَةَ قُرُونٍ.

Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alifariki mmoja kati ya mabinti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akatoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Muosheni mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, mkiona kuna haja ya kuzidisha, kwa maji na mkunazi, na mwisho muweka kafuri -au chochote katika kafuri-, mkimaliza nipeni idhini" Anasema: tulipomaliza tulimpa idhini, akatupatia kikoi chake, akasema: "Mfunikeni kwa kikoi hiki", anasema: Na tukafanya (nywele za) kichwa chake kuwa mafungu matatu.

Daraja: Sahihi

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 22

Kuingia Peponi kwa Kutekeleza Faradhi

عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَجُلاً سَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: أَرَأَيْتَ إِذَا صَلَّيْتُ الْمَكْتُوبَاتِ، وَصُمْتُ رَمَضَانَ، وَأَحْلَلْتُ الْحَلاَلَ، وَحَرَّمْتُ الْحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ عَلَى ذَلِكَ شَيْئاً، أَأَدْخُلُ الْجَنَّةَ؟ قَالَ: «نَعَمْ».

Kutoka kwa Abu Abdullah Jabir bin Abdullah al-Ansari (Radhi za Allah ziwe juu yao) kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume: Je, unaonaje nikiswali swala za faradhi, nikafunga Ramadhani, nikahalalisha halali na nikaharamisha haramu, bila kuzidisha kitu kingine chochote, je, nitaingia Peponi? Mtume akamjibu: "Ndio."

Daraja: Sahihi