Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 42%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

alituhadithiahukusanywaarobainikuandikamalaikamatendomkwelimwenyerizikipeponimotoniradhikishapandenyamamanne

Sahih al-Bukhari · Na. HE-66513

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ الصَّادِقُ المَصْدُوقُ: «إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ المَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَوْ سَعِيدٍ؛ فَوَالَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا، وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا».

Imepokewa kutoka kwa Abuu Abdirahman Abdullahi Bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alituhadithia Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye ndiye mkweli mwenye kusadikika: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake ndani ya tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu kwa mfano wake, kisha linakuwa pande la nyama mfano wake (siku arobaini), kisha linatumiwa Malaika analipulizia roho, na anaamrishwa kuandika maneno manne: Kuandika riziki yake, na umri wake, na matendo yake, na kuwa ni muovu au mwema; namuapa yule ambaye hakuna Mola isipokuwa yeye hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa Peponi mpaka ikawa baina yake na Peponi ni dhiraa moja (futi) kikamtangulia kitabu akafanya amali za watu wa motoni akauingia, na hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa motoni mpaka ikawa baina yake na Moto isipokuwa dhiraa, kitabu kikamtangulia akafanya amali za watu wa Peponi na akaingia".

Daraja: Sahihi

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 4

Hatua za Kuumbwa na Jaaliwa

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: «إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْماً نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إِلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٌّ أَوْ سَعِيدٌ...».

Kutoka kwa Abu Abdulrahman Abdullah bin Mas'ud (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Alituhadithia Mjumbe wa Allah (Rehema na amani za Allah ziwe juu yake), naye ni mkweli mwenye kusadikiwa: "Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake tumboni mwa mamaye kwa siku arobaini akiwa tone la manii, kisha huwa pande la damu kwa muda kama huo, kisha kipande cha nyama kwa muda kama huo. Kisha hutumwa malaika kwake na akampulizia roho, na akaamrishwa kuandika mambo manne: riziki yake, muda wa maisha yake, matendo yake, na kama atakuwa mtu wa motoni au wa peponi..."

Daraja: Sahihi