Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 43%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

nilichomfaradhishianinachokipendanimemtangaziaanaotembeleaakiniombakipenzinitampachangukwanguradhiuaduiwanguzaidisunnamkono

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 38

Kujikurubisha kwa Allah na Ulinzi wa Marafiki wa Allah (Awliyaa)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِيّاً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُهُ عَلَيْهِ، وَلاَ يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَلَئِنْ سَأَلَنِي لأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنِ اسْتَعَاذَنِي لأُعِيذَنَّهُ».

Kutoka kwa Abu Hurairah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mjumbe wa Allah amesema: "Hakika Allah Ta'ala amesema: Yeyote anayemfanyia uadui kipenzi Changu (walii wangu), basi nimemtangazia vita. Na mja Wangu hajikurubishi Kwangu kwa kitu Ninachokipenda zaidi kama kile Nilichomfaradhishia. Na mja Wangu ataendelea kujikurubisha Kwangu kwa amali za sunna mpaka Nimpende; Nikimpenda Ninakuwa masikio yake anayosikilizia, macho yake anayoonea, mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea. Akiniomba hakika Nitampa, na akijikinga Kwangu hakika Nitamkinga."

Daraja: Sahihi

Sahih al-Bukhari · Na. 6502

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُول اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقْد آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وما يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ».

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi hakika nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja wangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko kile nilichomfaradhishia, na hatoacha mja wangu kuendelea kujiweka karibu yangu kwa mambo ya sunna mpaka nitampenda, nikishampenda nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analoonea, na mkono wake anaokamatia, na mguu wake anaotembelea, na akiniomba hakika nitampa, na akinitaka ulinzi hakika nitamlinda".

Daraja: Sahihi