Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 18%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

kumwaminimjumbemwenyeradhi

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 15

Kusema Mazuri au Kunyamaza na Kuheshimu Wageni

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جَارَهُ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ».

Kutoka kwa Abu Hurairah (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mjumbe wa Allah amesema: "Mwenye kumwamini Allah na Siku ya Mwisho aseme mazuri au anyamaze, na mwenye kumwamini Allah na Siku ya Mwisho amkirimu jirani yake, na mwenye kumwamini Allah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake."

Daraja: Sahihi

Sahih Muslim · Na. 1885

Hukumu za Swala na Tohara

عن أبي قتادة الحارث بن رِبْعِيِّ رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم : أَنَّهُ قامَ فيهم، فذكرَ لهم أَنَّ الجهادَ في سبيلِ اللهِ، والإيمانَ باللهِ أفضلُ الأعمالِ، فقامَ رَجُلٌ، فقال: يا رسولَ اللهِ، أرأيتَ إن قُتِلْتُ في سبيلِ اللهِ، تُكَفَّرُ عَنِّي خَطَايَايَ؟ فقالَ له رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : «نعم، إنْ قُتِلْتَ في سبيلِ اللهِ، وأنتَ صَابِرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيْرُ مُدْبِرٍ». ثم قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : «كَيْفَ قُلْتَ؟» قال: أَرَأَيتَ إنْ قُتِلْتُ في سَبِيلِ اللهِ، أَتُكَفَّرُ عَنِّي خَطَايَايَ؟ فقالَ له رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : «نعم، وأنتَ صَابِرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيْرُ مُدْبِرٍ، إلا الدَّيْنَ؛ فَإنَّ جِبْرِيلَ -عليه السلام- قالَ لِي ذَلِكَ».

Kutoka kwa Abii Qatada Haritha bin Ribiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye alisimama kati yao, akawaeleza kuwa kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kumwamini Mweyezi Mungu ndio matendo bora, akasimama bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia: "Ndiyo, ikiwa utauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu na wewe ukiwa ni mwenye subira na kutaraji malipo ukiwa mstari wa mbele pasi na kurudi nyuma" Kisha akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Umesema vipi?" Akasema: Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia: "Ndiyo, ikiwa utauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu na wewe ukiwa ni mwenye subira na kutaraji malipo ukiwa mstari wa mbele pasina kurudi nyuma, isipokuwa deni; kwani Jibrili ziwe juu yake Amani kanieleza hivyo mimi".

Daraja: Sahihi