Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. HE-4177

Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَثَلُ الَّذِي يَذْكُرُ رَبَّهُ وَالَّذِي لاَ يَذْكُرُ رَبَّهُ، مَثَلُ الحَيِّ وَالمَيِّتِ»، ولفظ مسلم: «مَثَلُ الْبَيْتِ الَّذِي يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ، وَالْبَيْتِ الَّذِي لَا يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ، مَثَلُ الْحَيِّ وَالْمَيِّتِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Na kutoka kwa Abuu Musa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa", Na tamko la Muslim: "Mfano wa nyumba anayotajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na nyumba asiyotajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa".

English translation

Abu Mūsa (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The example of the one who remembers his Lord and the one who does not remember His Lord is like the example of the living and the dead person." The wording of Muslim reads: "The example of the house in which Allah is remembered and the house in which Allah is not remembered is like the example of the living and the dead person."

Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake tofauti kati ya yule anayemtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na kati ya yule asiyemtaja, kuwa ni mfano wa tofauti iliyopo kati ya aliyehai na aliyekufa katika manufaa yake na uzuri wa muonekano wake, hivyo mfano wa yule anayemtaja Mola wake ni mfano wa aliyehai ambaye muonekano wake umependeza kwa kuwa na nuru ya uhai, na anamanufaa, na mfano wa yule asiyemtaja Mwenyezi Mungu ni mfano wa maiti ambaye muonekano wake umeharibika, na ndani yake kumebatilika, na hana manufaa ndani yake. Na vile vile nyumba inasifiwa kwa sifa ya kuwa hai endapo wakazi wake wanamtaja Mwenyezi Mungu, na vinginevyo itakuwa nyumba mfu kwa kubweteka wakazi wake na kutomtaja Mwenyezi Mungu; na nyumba ikiitwa hai na maiti wanakusudiwa wakazi wa nyumba hiyo.

Faida

  • Himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu na tahadhari ya kughafilika na hilo.
  • Dhikri ndio uhai wa roho kama ambavyo roho ni uhai wa mwili.
  • Katika muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kupiga mifano ili kusogeza karibu maana.
  • Amesema Imam Nawawi: Hapa kuna wito wa kuja katika kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya nyumba, nakuwa haiachwi tupu pasina kumtaja Mwenyezi Mungu.
  • Amesema Nawawi: Na pia kuwa na umri mrefu katika utiifu ni fadhila hata ikiwa maiti atahama kwenda katika kheri zaidi; kwa sababu aliyehai anampata na kumzidi kwa yale anayoyafanya katika mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)