Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 6069

Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «كُلُّ أُمَّتِي مُعَافًى إِلَّا المُجَاهِرِينَ، وَإِنَّ مِنَ المُجَاهَرَةِ أَنْ يَعْمَلَ الرَّجُلُ بِاللَّيْلِ عَمَلًا، ثُمَّ يُصْبِحَ وَقَدْ سَتَرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ، فَيَقُولَ: يَا فُلاَنُ، عَمِلْتُ البَارِحَةَ كَذَا وَكَذَا، وَقَدْ بَاتَ يَسْتُرُهُ رَبُّهُ، وَيُصْبِحُ يَكْشِفُ سِتْرَ اللَّهِ عَنْهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi, na hakika miongoni mwa kutangaza machafu, ni mtu kutenda dhambi usiku, kisha akaamka akiwa kasitiriwa na Mwenyezi Mungu juu ya dhambi hilo, akaanza kusema: We fulani, jana usiku mimi nilifanya kadhaa wa kadhaa, hali yakuwa alilala usiku kucha Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka asubuhi anafunua pazia la Mwenyezi Mungu".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that he heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "All of my Ummah may be forgiven except those who commit sin openly. One kind of committing sin openly is when one commits something during the night, then the morning comes and Allah has screened it, but he says: 'O So-and-so, last night, I did such-and-such.' Though he spent the night screened by his Lord (none knowing about his sin), in the morning he removes Allah's screen from himself."

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu mtenda dhambi anatarajiwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu, isipokuwa mwenye kutangaza maasi kwa kutaka ufahari na jeuri, huyu hastahiki msamaha; anafanya maasi mchana, kisha anaamka hali yakuwa Mwenyezi Mungu kamsitiri, anaanza kumsimulia mwingine kuwa yeye jana alifanya maasi fulani, na hali yakuwa alilala Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka anafunua pazia la Mwenyezi Mungu juu yake!!.

Faida

  • Ubaya wa kuweka wazi maasi baada ya kusitiriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Katika kutangaza maasi ni kusambaza machafu baina ya waumini.
  • Mwenye kusitiriwa na Mwenyezi Mungu duniani atamsitiri pia Akhera, na hii ni katika upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake.
  • Atakayepata mtihani wa maasi, anatakiwa ajifiche, na atubie kwa Mwenyezi Mungu.
  • Ukubwa wa dhambi la kutangaza madhambi kwa wale wanaokusudia kuweka wazi maasi, na wanajikosesha wao wenyewe kusamehewa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)