Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-3389

Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَن عَبدِ الله بنِ الشِّخِّير رضي الله عنه قَالَ: انْطَلَقْتُ في وَفدِ بَنِي عَامِرٍ إِلى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقُلنا: أَنتَ سيّدُنَا، فقال: «السَّيدُ اللهُ»، قُلنا: وَأَفْضَلُنا فَضْلاً، وأعظَمُنا طَوْلاً، فقال: «قُولُوا بِقَولِكُم، أَو بَعضِ قولِكُم، وَلَا يَسْتَجْرِيَنَّكُم الشَّيطَانُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Shikhiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisafiri katika msafara wa Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani".

English translation

‘Abdullah ibn ash-Shikhkhīr (may Allah be pleased with him) reported: I set out with the delegation of Banu ‘Āmir to meet the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him). We said: You are our master. He said: "The Master is Allah." We said: And the best of us in superiority and the greatest among us in bounty. He said: "Say what you have to say, or part of what you have to say, but do not let the devil deviate you (in praising me)."

Maelezo

Lilikuja kundi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, walipofika kwake wakasema -kwa kumsifu- kwa baadhi ya maneno ambayo aliyachukia -Rehema na amani ziwe juu yake-, Wakasema: "Wewe ni bwana yetu", Akasema kuwaambia -Rehema na amani ziwe juu yake- "Bwana ni Mwenyezi Mungu" Yeye ndiye mwenye ubwana uliokamilika juu ya viumbe wake nao ni waja wake. Na wakasema: "Wewe ndiye mbora wetu" na mwenye daraja na utukufu wa juu kuliko sisi na mwenye sifa nyingi. Na wewe "Ndiye mtoaji zaidi kuliko sisi" na mwingi wa ukarimu na utukufu na daraja ya juu. Kisha akawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake waseme kauli yao iliyozoeleka na wasijilazimishe kutafuta maneno mengine, na kuwa shetani asiwavute katika kuchupa mipaka na kupitiliza kunakopelekea kuingia katika yale yaliyoharamishwa miongoni mwa shirki na njia zake.

Faida

  • Utukufu wa cheo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndani ya nafsi za Masahaba wake na heshima yao kwake.
  • Katazo la kijikalifisha katika matamshi, na kubakia katika maneno yaliyozoeleka.
  • Kuilinda tauhidi dhidi ya yale yanayoiharibu miongoni mwa kauli na matendo.
  • Katazo la kuchupa mipaka katika kusifu, kwani hilo ni katika njia za Shetani.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndiye bwana wa watoto wa Adam, na haya yaliyotajwa katika hadithi hii ni katika sehemu ya unyenyekevu, na ni katika sehemu ya kuwahofia wao wasijekuchupa mipaka katika hilo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)