Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-3383

Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسعودٍ رضي الله عنه عن رَسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال: «الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، -ثلاثًا-»، وَمَا مِنَّا إِلَّا، وَلَكِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يُذْهِبُهُ بِالتَّوَكُّلِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea.

English translation

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Tiyarah (belief in evil omens) is Shirk (polytheism). Tiyarah is Shirk. Tiyarah is Shirk - three times." Every one of us experiences something of that, but Allah Almighty dispels it with reliance on Him.

Maelezo

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na imani ya mikosi: Nayo ni kuamini mikosi ya chochote chenye kusikika au chenye kuonekana, kama ndege au wanyama au walemavu au namba au siku au kinginecho, Na bila shaka ametaja ndege kwa sababu ndio ilikuwa maarufu kipindi cha zama za ujinga, na asili yake ni kumuachia ndege aruke katika jambo kama safari au biashara au kinginecho, akiruka pande wa kulia anajipa bishara na anatekeleza anachotaka kukifanya, na akirukia upande wa kushoto, anaamini ni mkosi na anaacha kufanya alichotaka kukifanya. Na akaeleza kuwa kitendo hicho ni ushirikina, na mikosi imekuwa ni ushirikina kwa sababu hakuna aletaye kheri ila Mwenyezi Mungu, na wala hazuii shari ila Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika. Na ametaja bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake kuwa inaweza kuingia katika moyo wa muislamu kiasi kidogo cha imani ya mkosi, lakini anatakiwa akizuie kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, ikiwa ni pamoja na kufanya sababu.

Faida

  • Mikosi ni ushirikina; kwa sababu ndani yake kuna kuufungamanisha moyo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
  • Umuhimu wa kurudia mambo muhimu, ili yahifadhike na yakite ndani ya moyo.
  • Mikosi huondolewa kwa kutegemea kwa Allah Mtukufu.
  • Amri ya kutegemea kwa Allah pekee na moyo kufungamana naye Mtukufu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)