Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2622

Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «رُبَّ أَشْعَثَ مَدْفُوعٍ بِالْأَبْوَابِ لَوْ أَقْسَمَ عَلَى اللهِ لَأَبَرَّهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Perhaps a disheveled, rejected person at the doors, if he were to swear by Allah, He would fulfill his oath."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kuna baadhi ya watu wana nywele zilizoshikana tena zilizojaa vumbi, na hawazipaki mafuta wala hajali kuziosha, na wala hawana heshima yoyote mbele za watu, basi watu humsukuma mtu kama huyu katika milango yao, na kumfukuza kwa kumdharau; isipokuwa mtu huyu lau angeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa litokee jambo basi Mwenyezi Mungu angelitenda jambo hilo kwa sababu ya kumkirimu na kumtukuza kwa kujibu ombi lake, na kumlinda asijekupotoka katika kiapo chake, na hii ni kwa sababu ya ubora wake na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Mwenyezi Mungu hatazami sura ya mja, lakini anatazama ndani ya nyoyo na matendo.
  • Ni jukumu la kila mtu kuyapa kipaumbele matendo yake na usafi wa moyo wake zaidi kuliko kuutilia maanani mwili wake na mavazi yake.
  • Kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu na kujidhalilisha kwake ni sababu ya kujibiwa dua, na ndiyo maana; Mwenyezi Mungu hukiepusha kuanguka patupu kiapo cha wachamungu na wenye maisha duni.
  • Kumebainishwa malezi ya kiutume kwa watu; ili wasidharauliane wao kwa wao.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)