Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: «اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْهُدَى وَالتُّقَى، وَالْعَفَافَ وَالْغِنَى».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka".
English translation
‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) used to say: "Allāhumma inni as’aluka al-huda wa at-tuqa wa al-‘afāf wa al-ghina (O Allah, I ask You for guidance, piety, chastity, and self-sufficiency)."
Maelezo
Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uongofu" na njia iliyonyooka katika kuijua haki na kuifanyia kazi, "na uchamungu", kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo, "na kujizuia na machafu" kujizuia na yale yasiyokuwa halali wala si mazuri miongoni mwa kauli au kitendo, "na kutosheka" na viumbe, kiasi ambacho asimuhitaji yeyote zaidi ya Mola wake Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.
Faida
- Utukufu wa mambo haya: Uongofu, uchamungu, na kujizuia na machafu, na kutosheka, na himizo la kujipamba nayo.
- Mtume rehema na amani ziwe juu yake hamiliki juu ya nafsi yake manufaa wala madhara, na kwamba anayemiliki hayo ni Allah Mtukufu.
- Anayemiliki manufaa na madhara na uongofu kwa viumbe ni Mwenyezi Mungu peke yake, si Malaika aliyekaribu wala Mtume aliyetumwa wala yeyote asiyekuwa wao.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.