Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 486

Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: فَقَدْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيْلَةً مِنَ الْفِرَاشِ فَالْتَمَسْتُهُ فَوَقَعَتْ يَدِي عَلَى بَطْنِ قَدَمَيْهِ وَهُوَ فِي الْمَسْجِدِ وَهُمَا مَنْصُوبَتَانِ، وَهُوَ يَقُولُ: «اللهُمَّ أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقُوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ لَا أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"

English translation

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: One night I did not find the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) in bed, and as I groped for him, my hand fell over the sole of his feet, while he was in the mosque, and they were held erect. He was saying: "O Allah, I seek refuge with Your pleasure from Your wrath, and with Your pardon from Your punishment, and I seek refuge with You from You. I cannot enumerate praise of you; You are as You have praised Yourself."

Maelezo

Anasema Aisha radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nimelala pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamkosa wakati wa usiku, nikagusa kwa mkono wangu sehemu aliyokuwa akiswalia ndani ya chumba; ghafla nikamuona amesujudu na miguu yake ikiwa imesimamishwa, mara nikamsikia akisema: "Ninajilinda" Na ninapitia "Katika radhi zako dhidi ya hasira zako" juu yangu au juu ya umma wangu, "na" ninaomba kinga "kwa salama yako" na msamaha wako mwingi "kutokana na adhabu zako", "na ninajilinda kwako kutokana nawe" na kwa sifa za uzuri wako kutokana na sifa za utukufu wako, kiasi kwamba hakuna awezaye kukinga dhidi yako ila wewe, hakuna pa kusalimika wala pa kujilinda kutokana na Mwenyezi Mungu ila kwake, "Siwezi kuzihesabu sifa zako" Sina uwezo wala siwezi kufikia kuzidhibiti na kuzihesabu kwa idadi kwa kushindwa kwangu kuzidhibiti kwa wingi neema zako na ihisani yako kama unavyostahiki, hata kama nikijitahidi katika hilo, "Wewe kama ulivyoisifia nafsi yako" wewe ndiye uliyeisifu dhati yako sifa zinazokustahiki, ni nani awezaye kutimiza haki ya sifa zako?!

Faida

  • Sunna ya kuomba dua hii katika sijida.
  • Amesema Miriki: Na katika moja kati ya riwaya za Nasaai: Alikuwa akisema dua hii anapomaliza swala yake na akaelekea kitandani kwake.
  • Sunna ya kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa zake na kumuomba kwa majina yake yaliyothibiti katika Qur'ani na Sunna.
  • Hapa kuna kumtukuza muumba wakati wa kurukuu na kusujudu.
  • Inafaa kuomba ulinzi kupitia sifa za Mwenyezi Mungu, kama ambavyo inafaa kuomba ulinza kupitia dhati yake Yeye Aliyetakasika na kutukuka.
  • Amesema Al-Khattwabi: Katika maneno haya kuna maana ya ndani sana, nayo: Nikuwa aliomba kinga kwa Mwenyezi Mungu amkinge kupitia radhi zake kutokana na hasira zake, na kwa salama yake dhidi ya adhabu zake, na ridhaa na hasira ni maneno mawili tofauti yanayokwenda sambamba, vile vile kusalimika na kuadhibiwa pia, alipofikia kumtaja ambaye hana kinyume chake ambaye ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alitaka kinga kutokana na Yeye kwake mwenyewe na si kwa mwingine, na maana yake: Ni kuomba msamaha dhidi ya mapungufu ya kutofikia wajibu wa haki stahiki katika kumuabudu, na kumtukuza. Na kauli yake: Sizidhibiti sifa juu yako: Yaani sina uwezo wala siwezi kuzifikia.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)