Nyuma

Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: فَقَدْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيْلَةً مِنَ الْفِرَاشِ فَالْتَمَسْتُهُ فَوَقَعَتْ يَدِي عَلَى بَطْنِ قَدَمَيْهِ وَهُوَ فِي الْمَسْجِدِ وَهُمَا مَنْصُوبَتَانِ، وَهُوَ يَقُولُ: «اللهُمَّ أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقُوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ لَا أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ».

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: One night I did not find the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) in bed, and as I groped for him, my hand fell over the sole of his feet, while he was in the mosque, and they were held erect. He was saying: "O Allah, I seek refuge with Your pleasure from Your wrath, and with Your pardon from Your punishment, and I seek refuge with You from You. I cannot enumerate praise of you; You are as You have praised Yourself."

Sunna ya kuomba dua hii katika sijida.

Amesema Miriki: Na katika moja kati ya riwaya za Nasaai: Alikuwa akisema dua hii anapomaliza swala yake na akaelekea kitandani kwake.

Sunna ya kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa zake na kumuomba kwa majina yake yaliyothibiti katika Qur'ani na Sunna.

Hapa kuna kumtukuza muumba wakati wa kurukuu na kusujudu.

Inafaa kuomba ulinzi kupitia sifa za Mwenyezi Mungu, kama ambavyo inafaa kuomba ulinza kupitia dhati yake Yeye Aliyetakasika na kutukuka.

Amesema Al-Khattwabi: Katika maneno haya kuna maana ya ndani sana, nayo: Nikuwa aliomba kinga kwa Mwenyezi Mungu amkinge kupitia radhi zake kutokana na hasira zake, na kwa salama yake dhidi ya adhabu zake, na ridhaa na hasira ni maneno mawili tofauti yanayokwenda sambamba, vile vile kusalimika na kuadhibiwa pia, alipofikia kumtaja ambaye hana kinyume chake ambaye ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alitaka kinga kutokana na Yeye kwake mwenyewe na si kwa mwingine, na maana yake: Ni kuomba msamaha dhidi ya mapungufu ya kutofikia wajibu wa haki stahiki katika kumuabudu, na kumtukuza. Na kauli yake: Sizidhibiti sifa juu yako: Yaani sina uwezo wala siwezi kuzifikia.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 486 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:3566