Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-3336

Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم: «اللهُمَّ لَا تَجْعَلْ قَبْرِي وَثَنًا، لَعَنَ اللهُ قَوْمًا اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "O Allah, do not make my grave an idol that is worshiped. Allah cursed the people who took the graves of their prophets as places of worship."

Maelezo

Alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mola wake asilifanye kaburi lake kuwa mithili ya sanamu lenye kuabudiwa na watu kwa kulitukuza, na kulielekea wakati wa kusujudu; kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi mungu yuko mbali na amemumfukuza na kumtowa kwenye rehema zake yeyote atakaye fanya makaburi ya manabii kuwa ni misikiti,kwani kulifanya kuwa msikiti ni njia ya kuelekea kuliabudu na kuliitakidi hivyo.

Faida

  • Kuvuka mpaka wa kisheria katika makaburi ya Manabii na watu wema hufanya yaabudiwe kinyume na Mwenyezi Mungu, ni lazima kuchukua tahadhari na njia zinazopelekea katika ushirikina.
  • Haifai kwenda makaburini kwa lengo la kuyatukuza na kufanya ibada hapo, vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wa mwenye kaburi na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi.
  • Uharamu wa kuswali makaburini hata kama hujajengwa msikiti hapo, isipokuwa swala ya jeneza ambalo halijaswaliwa (wanaweza kuswalia kwa dharura hiyo)

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)