Nyuma

Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم: «اللهُمَّ لَا تَجْعَلْ قَبْرِي وَثَنًا، لَعَنَ اللهُ قَوْمًا اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ».

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "O Allah, do not make my grave an idol that is worshiped. Allah cursed the people who took the graves of their prophets as places of worship."

Kuvuka mpaka wa kisheria katika makaburi ya Manabii na watu wema hufanya yaabudiwe kinyume na Mwenyezi Mungu, ni lazima kuchukua tahadhari na njia zinazopelekea katika ushirikina.

Haifai kwenda makaburini kwa lengo la kuyatukuza na kufanya ibada hapo, vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wa mwenye kaburi na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi.

Uharamu wa kuswali makaburini hata kama hujajengwa msikiti hapo, isipokuwa swala ya jeneza ambalo halijaswaliwa (wanaweza kuswalia kwa dharura hiyo)

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Musnad Ahmad · Hadith Na. HE-3336 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
ahmad:hadeethenc:3336