Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2592

Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ جَرِيرٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ يُحْرَمِ الرِّفْقَ يُحْرَمِ الْخَيْرَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote"

English translation

Jarīr (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "He who is deprived of gentleness is deprived of goodness."

Maelezo

Anatueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunyimwa upole akawa hakuafikishwa katika mambo ya dini na dunia, na katika mambo yake mwenyewe, na yale anayoyafanya na wengine, basi atakuwa kanyimwa kheri yote.

Faida

  • Fadhila za upole na himizo la kujipamba na tabia hiyo, na kemeo la ukali.
  • Upole hunyoosha kheri za Dunia na Akhera na hupanua mlango wa baraka, lakini ukali ni kinyume chake.
  • Upole ni taji ambalo hutokana na tabia njema na amani, na jeuri hutokana na hasira na ufidhuli, ndio maana aliusifia sana upole Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapitiliza katika kusifu.
  • Alisema Sufian Al-Thauri Mwenyezi Mungu amrehemu, akiwaambia jamaa zake: Je, mnajua upole ni nini? Ni kuweka mambo mahali pake panapofaa, na ukali mahali pake panapofaa, na upole mahali pake panapofaa, upanga mahali pake panapofaa, na mjeledi mahali pake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)