Nyuma

Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ جَرِيرٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ يُحْرَمِ الرِّفْقَ يُحْرَمِ الْخَيْرَ».

Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote"

Jarīr (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "He who is deprived of gentleness is deprived of goodness."

Fadhila za upole na himizo la kujipamba na tabia hiyo, na kemeo la ukali.

Upole hunyoosha kheri za Dunia na Akhera na hupanua mlango wa baraka, lakini ukali ni kinyume chake.

Upole ni taji ambalo hutokana na tabia njema na amani, na jeuri hutokana na hasira na ufidhuli, ndio maana aliusifia sana upole Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapitiliza katika kusifu.

Alisema Sufian Al-Thauri Mwenyezi Mungu amrehemu, akiwaambia jamaa zake: Je, mnajua upole ni nini? Ni kuweka mambo mahali pake panapofaa, na ukali mahali pake panapofaa, na upole mahali pake panapofaa, upanga mahali pake panapofaa, na mjeledi mahali pake.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 2592 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:hadeethenc:4939