Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1955

Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن شداد بن أوس رضي الله عنه قال: ثِنْتَانِ حَفِظْتُهُمَا عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، فَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa Kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mambo mawili niliyahifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu, mtakapoua basi ueni kwa namna iliyokuwa nzuri, na mtakapochinja basi kwa namna iliyokuwa nzuri, na anoe mmoja wenu zana yake ya kuchinjia, na akistareheshe kichinjwa chake".

English translation

Shaddād ibn Aws (may Allah be pleased with him) reported: There are two things which I learned by heart from the Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him); he said: "Verily, Allah has enjoined kindness in all things. So, when you kill, kill with kindness; and when you slaughter, slaughter with kindness. Let one of you sharpen his blade and spare the animal he slaughters from suffering."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja. Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa. Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.

Faida

  • Huruma ya Mwenyezi Mungu na upole wake kwa viumbe.
  • Wema wa kuuwa na kuchinja uwe kwa namna ya kisheria.
  • Ukamilifu wa sheria na kushughulikia kwake kila kheri, na miongoni mwake ni kuwahurumia wanyama na upole juu yao.
  • Katazo la kusulubu (kumtesa) mwanadamu baada ya kumuua.
  • Uharamu wa kila chenye kumtesa mnyama.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)