Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 3480

Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «كان رجلٌ يُدَايِنُ الناسَ، فكان يقول لفتاه: إذا أتيتَ مُعسِرًا فتجاوز عنه، لعل اللهَ يَتجاوزُ عنا، فلقي اللهَ فتجاوز عنه».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe (alipokufa) akakutana na Allah, akamsamehe".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There was a man who used to give loans to people. He would say to his servant: ‘When you come to an insolvent person, overlook his debt; perhaps Allah would overlook our sins.’ So, the man met Allah (after death), and He overlooked his sins."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuhusu bwana mmoja aliyekuwa akiamiliana na watu kwa mkopo, au akiwauzia kwa mkopo, Na alikuwa akisema kumwambia kijana wake aliyekuwa akikusanya madeni yaliyoko kwa watu: Utakapomwendea mdaiwa na akawa hana cha kulipa deni analodaiwa kwa sababu ya kushindwa "Basi, msamehe"; Ima kwa kumpa muda zaidi na kutong'ang'ania kumdai, Au kwa kukubali alichonacho hata kama kina mapungufu, na hiyo ni kwa hamu yake na tamaa yake ya kutaka Allah asimuadhibu na amsamehe, Alipofariki Allah akamsamehe na hakumuadhibu kwa makosa yake mengine.

Faida

  • Wema katika kuamiliana na watu na kuwasamehe na kumpa uhuru mwenye hali ngumu ni katika sababu kubwa za mja kusalimika siku ya Kiyama.
  • Kuwafanyia wema viumbe na kutakasa matendo kwa ajili ya Allah na kutaraji katika rehema zake ni katika sababu za kupata msamha wa madhambi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)