Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عن جابر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «رَحِمَ اللهُ رَجُلًا سَمْحًا إِذَا بَاعَ، وَإِذَا اشْتَرَى، وَإِذَا اقْتَضَى».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni".
English translation
Jābir (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "May Allah have mercy on a man who is lenient when he sells, when he buys, and when he asks for repayment of the debt."
Maelezo
Alimuombea rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila mwenye kuwa mwepesi mkarimu mpole katika biashara yake; Hamkadamizi mnunuzi katika bei yake, na anaamiliana naye kwa tabia njema, Mwepesi mkarimu mpole anaponunua; Hapunji na kupunguza thamani ya bidhaa, Mwepesi mkarimu mpole anapodai kulipwa madeni yake; hamtilii mkazo fukara na muhitaji, bali anamdai kwa upole na huruma, na anampa muda mwenye hali ngumu.
Faida
- Miongoni mwa malengo ya sheria ni kuhifadhi yenye kutengeneza mahusiano baina ya watu.
- Himizo la kutumia tabia za hali ya juu katika miamala baina ya watu kuanzia kuuza na kununuwa na mfano wake.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.