Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 5641

Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «مَا يُصِيبُ الْمُسْلِمَ مِنْ نَصَبٍ وَلَا وَصَبٍ وَلَا هَمٍّ وَلَا حُزْنٍ وَلَا أَذًى وَلَا غَمٍّ حَتَّى الشَّوْكَةِ يُشَاكُهَا إِلَّا كَفَّرَ اللهُ بِهَا مِنْ خَطَايَاهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake."

English translation

Abu Sa‘īd al-Khudri and Abu Hurayah (may Allah be pleased with both of them) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "No fatigue, disease, sorrow, sadness, harm, or distress befalls a Muslim, even if it were a prick of a thorn, but Allah will expiate some of his sins thereby."

Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yanayomsibu muislamu katika maradhi na msongo na huzuni na misukosuko na majanga na shida mbali mbali na hofu na njaa, hata kama utakuwa ni mwiba utakaomchoma na kumuumiza, hilo kwake linakuwa ni kafara ya madhambi kwake na kifuta makosa.

Faida

  • Kumebainishwa fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waumini na huruma yake kwao kwa kuwasamehe madhambi hata kwa madhara madogo yanayowasibu.
  • Ni lazima kwa muislamu ataraji malipo kwa Allah kwa yale yanayomsibu, na asubiri kwa dogo na kubwa, ili iwe ni sababu ya kunyanyuliwa daraja na ni kafara ya makosa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)