Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 6488

Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «الْجَنَّةُ أَقْرَبُ إِلَى أَحَدِكُمْ مِنْ شِرَاكِ نَعْلِهِ، وَالنَّارُ مِثْلُ ذَلِكَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa Kutoka kwa Ibn Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo".

English translation

Ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Paradise is nearer to one of you than his shoelaces, and so is Hellfire."

Maelezo

Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Pepo na Moto viko karibu mno na mwanadamu kama ukaribu wa mwendo wa kiatu unaokuwa juu ya kisigino, kwa sababu anaweza kufanya twa'a (ibada) katika yale yanayomridhisha Allah Mtukufu akaingia Peponi kwa ibada hiyo, au dhambi moja likawa sababu ya kuingia motoni.

Faida

  • Himizo la kufanya heri hata kama ni ndogo, na tishio la kufanya shari hata kama ni ndogo.
  • Ni lazima muislamu katika maisha yake kukusanya kati ya kutaraji mazuri na kuogopa adhabu, na kumuomba Allah Mtukufu muda wote kuthubutu (Kudumu) katika haki mpaka asalimike na wala asihadaike na hali aliyonayo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)