Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. 3681

Kinacholewesha kikiwa kingi, basi hata kidogo ni haramu

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا أَسْكَرَ كَثِيرُهُ فَقَلِيلُهُ حَرَامٌ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Jaabir bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Kinacholewesha kikiwa kingi, basi hata kidogo ni haramu".

English translation

Jābir ibn ‘Abdullah (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whatever intoxicates in large amounts, its small amount is forbidden."

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa kila kinywaji au chakula kinachoondosha akili wakati wa kukitumia kingi chake, basi kukitumia kidogo chake ni haramu, hata kisipoondosha akili.

Faida

  • Sheria imehifadhi akili za watu.
  • Kufaa kuzingatia mlango wa kuzuia sababu zinazopelekea katika maovu, na hiyo ni kwa kufunga kila njia inayopelekea katika machafu hayo.
  • Kumeharamishwa kichache katika kilevi; kwa sababu ndio njia ya kulewa.
  • Kisipolewesha si kidogo wala kingi, basi hicho si haramu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)