Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. 1052

Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ أَبِي الْجَعْدِ الضَّمْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ، وَكَانَتْ لَهُ صُحْبَةٌ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ تَرَكَ ثَلَاثَ جُمَعٍ تَهَاوُنًا بِهَا طَبَعَ اللَّهُ عَلَى قَلْبِهِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abul Ja'di Adh-dhwamri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa na uswahaba, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake"

English translation

Abu al-Ja‘d ad-Damri (may Allah be pleased with him), who had a companionship with the Prophet, reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever abandons three Fridays out of negligence, Allah seals his heart."

Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoacha swala ya Ijumaa, na kwamba mwenye kuacha swala ya Ijumaa mara tatu kwa kupuuza na uzembe pasina udhuru basi Mwenyezi Mungu atapiga na kufunika juu ya moyo wake na kizibo kinachozuia kuingia kheri yoyote ndani ya nafsi yake.

Faida

  • Ameeleza bin Mundhiri kuwa kuna makubaliano ya wanachuoni wote kuwa swala ya Ijumaa ni faradhi ya lazima kwa kila mtu.
  • Ahadi mbaya kwa atakayeacha swala ya Ijumaa kwa kupuuza, kwamba Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya moyo wake.
  • Atakayeacha swala ya Ijumaa kwa dharura huyu haingii katika ahadi hii mbaya.
  • Amesema Shaukani: Kauli yake: (Ijumaa tatu), inategemea maana mbili, kuacha kwa ujumla sawa sawa zimefuatana Ijumaa hizo au zimetofautiana, hata akiacha katika kila mwaka Ijumaa moja basi Mwenyezi Mungu angepiga muhuri juu ya moyo wake baada ya Ijumaa ya tatu, na ndivyo hadithi inavyoonyesha, na maana ya pili nikuwa inakusudiwa Ijumaa tatu mfululizo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)