Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عن أُمِّ عَطِيَّةَ رَضي الله عنها، وكَانَتْ بايَعَت النبيَّ صلى الله عليه وسلم، قالت: كُنَّا لا نَعُدّ الكُدرَةَ والصُّفْرَةَ بعدَ الطُّهرِ شيئًا.
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa kampa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: "Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote".
English translation
’Umm ‘Atiyyah (may Allah be pleased with her), the one who pledged allegiance to the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him), reported: After becoming pure (from menstruation), we would not consider brownish and yellowish discharges to be of any significance.
Maelezo
Ameeleza swahaba mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake kuwa wanawake katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walikuwa hawayazingatii maji maji yanayotoka katika tupu -ambayo yanaelekea katika weusi, au katika njano- baada ya kuona twahara ya kutoka katika hedhi: kuwa ni hedhi, hawaachi swala na swaumu kwa sababu yake.
Faida
- Maji maji yanayoshuka kutoka katika utupu wa mwanamke baada ya twahara ya hedhi hayazingatiwi hata kama yatakuwa na rangi ya kahawia au njano inayotokana na damu.
- Kushuka kwa maji maji ya kahawia au njano wakati wa hedhi na ada inazingatiwa kuwa ni hedhi; kwa sababu kwa wakati huo ni damu, ila tu inakuwa imechanganyikana na maji.
- Mwanamke haachi swala wala swaumu kwa sababu ya maji maji ya kahawia au ya njano yanayotoka baada ya twahara, bali atatawadha na ataswali.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.