Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. 2675

Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عنْ ابنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَانْطَلَقَ لِحَاجَتِهِ، فَرَأَيْنَا حُمَّرَةً مَعَهَا فَرْخَانِ، فَأَخَذْنَا فَرْخَيْهَا، فَجَاءَتِ الْحُمَرَةُ فَجَعَلَتْ تَفْرِشُ، فَجَاءَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «مَنْ فَجَعَ هَذِهِ بِوَلَدِهَا؟ رُدُّوا وَلَدَهَا إِلَيْهَا»، وَرَأَى قَرْيَةَ نَمْلٍ قَدْ حَرَّقْنَاهَا، فَقَالَ: «مَنْ حَرَّقَ هَذِهِ؟» قُلْنَا: نَحْنُ. قَالَ: «إِنَّهُ لَا يَنْبَغِي أَنْ يُعَذِّبَ بِالنَّارِ إِلَّا رَبُّ النَّارِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka kwa ajili ya haja yake, tukaona ndege akiwa na makinda mawili, tukawachukua makinda wake, akaja yule ndege akaanza kupepesa mbawa zake, basi akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ni nani aliyemuhuzunisha ndege huyu kwa mwanaye? Mrejesheeni mwanaye", na akaona kijiji cha wadudu chungu tulichokichoma kwa moto, akasema: "Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto".

English translation

Ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: We were on a journey with the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) when he went to relieve himself. We then saw a Hummarah (a type of bird) with its two chicks. We took its chicks, and the bird came back and began to flap its wings. Upon seeing it, the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) came and said: "Who has distressed it by taking its baby? Return its baby." He then saw an ant colony that we had burned, and he said: "Who burned this?" We said: We did. He said: "No one should punish with fire except the Lord of fire."

Maelezo

Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili kukidhi haja yake, Maswahaba zake wakapata ndege aina ya Hummara akiwa na makinda mawili, wakayachukua, yule ndege akaanza kupeperusha mbawa zake na kuzipepesa kwa huzuni kwa kuwakosa makinda wake, akaja rehema na amani ziwe juu yake na akasema: Ni nani aliyemuhuzunisha na akamuhofisha kwa kuchukua vitoto vyake? Kisha akaamrisha virejeshwe kwake. Kisha akaona kijiji cha wadudu chungu kilichochomwa kwa moto, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni nani aliyekiunguza hiki? Wakasema baadhi ya Maswahaba: Sisi. Akasema kuwaambia: Hakika haifai kwa yeyote kuadhibu kiumbe hai kwa moto; isipokuwa Mwenyezi Mungu muumba wake.

Faida

  • Sheria ya kujisitiri kwa ajili ya kukidhi haja.
  • Katazo la kuwaadhibu wanyama kwa kuchukua watoto wao.
  • Katazo la kuwachoma sisimizi na wadudu wengineo kwa moto.
  • Himizo la upole na huruma kwa wanyama, na Uislamu ndio ulitangulia kulisema hilo.
  • Huruma yake rehema na amani ziwe juu yake kwa wanyama.
  • Kuadhibu kwa moto ni miongoni mwa mambo anayohusika nayo Mola Mtukufu pekee.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)