Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1648

Msiape kwa masanamu, wala kwa baba zenu

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ سَمُرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَحْلِفُوا بِالطَّوَاغِي، وَلَا بِآبَائِكُمْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abdillahi bin Omari- radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiape kwa masanamu, wala kwa baba zenu"

English translation

‘Abdur-Rahmān ibn Samurah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Do not swear by Tawāghi (idols) nor by your fathers."

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kuapa kwa mashetani, yaani wingi wa shetani, nayo ni masanamu waliyokuwa wakiyaabudu washirikina badala ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo yalikuwa sababu ya ujeuri wao na ukafiri wao. Anakataza rehema na amani ziwe juu yake kuapa kwa baba za mtu; Ilikuwa ni desturi ya Waarabu katika zama za kabla ya Uislamu kuapa kwa baba zao kwa kujifaharisha na kwa kuwatukuza.

Faida

  • Hifai kuapa ila kwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake.
  • Uharamu wa kuapa kwa twaghuti, na mababa, na viongozi na masanamu, na mfano wa hayo katika kila batili.
  • Kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni katika shirki ndogo, na inaweza kuwa shirki kubwa, atakaposimama kwa moyo wake kumtukuza yule anayemuapia, nakuwa anamtukuza kama anavyomtukuza Mwenyezi Mungu au anaitakidi kuwa anastahiki sehemu katika ibada.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)