Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2113

Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَصْحَبُ الْمَلَائِكَةُ رُفْقَةً فِيهَا كَلْبٌ وَلَا جَرَسٌ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Angels do not accompany a group of travelers who have a dog or a bell with them."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hawafuatani na msafara katika safari, na ndani ya msafara kuna mbwa, au kengele inayotundikwa kwa wanyama ikitoa sauti mnyama anapotembea.

Faida

  • Katazo la kufuga mbwa na kusuhubiana nao, isipokuwa mbwa wa kuwinda au wa ulinzi.
  • Malaika wanaojizuia kufuatana na msafara ni Malaika wa rehema, ama wale waandika matendo hao hawamwachi mtu akiwa nyumbani au safarini.
  • Katazo la kengele; kwani ni zumari katika mazumari ya shetani, na kuna kujifananisha na Wakristo.
  • Ni juu ya muislamu kujiweka mbali na yale yote yanayowaweka Malaika mbali naye .

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)