Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 6213

Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la kipenzi chake mfano wa kuku anavyotetea, hulichanganya na uongo zaidi ya mia moja (100)

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن عائشة رضي الله عنها قالت: سَأَلَ أُنَاسٌ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْكُهَّانِ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسُوا بِشَيْءٍ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، فَإِنَّهُمْ يُحَدِّثُونَ أَحْيَانًا بِالشَّيْءِ يَكُونُ حَقًّا، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تِلْكَ الْكَلِمَةُ مِنَ الْحَقِّ يَخْطَفُهَا الْجِنِّيُّ فَيَقُرُّهَا فِي أُذُنِ وَلِيِّهِ قَرَّ الدَّجَاجَةِ، فَيَخْلِطُونَ فِيهَا أَكْثَرَ مِنْ مِائَةِ كَذْبَةٍ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Kuna watu walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu makuhani, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawana lolote" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika wao husimulia jambo baadhi ya nyakati na likawa kweli, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la kipenzi chake mfano wa kuku anavyotetea, hulichanganya na uongo zaidi ya mia moja (100)".

English translation

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: Some people asked the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) about diviners, and he said to them: "They are of no account." They said: "O Messenger of Allah, but they sometimes make true predictions." Thereupon, the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "That is a word pertaining to the truth which a jinn snatches and whispers into his friend's ears as a hen does. Then, they mix it with more than a hundred lies."

Maelezo

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wale wanaoeleza mambo yajayo yaliyofichikana, akasema: Msiwajali, na wala msiyachukue maneno yao, na wala msiyajali mambo yao. Wakasema: Hakika kauli yao huendana na uhalisia katika baadhi ya nyakati, kama ambavyo huelezea kutokea kwa jambo la gahibu ndani ya mwezi fulani siku fulani, na likatokea sambamba na kauli yao. Akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Hakika Majini huiba yale wanayoyasikia katika habari za mbinguni, wakashuka kuja kwa watu wao miongoni mwa makuhani wakawaeleza waliyoyasikia, kisha kuhani anaongeza katika yale aliyoyasikia kutoka mbinguni uongo mia moja (100).

Faida

  • Katazo la kuwasadikisha makuhani, nakuwa wanayoyasema ni uongo na uzushi, hata kama watasema ukweli katika baadhi ya nyakati.
  • Mbingu zimehifadhiwa dhidi ya Mashetani kwa kutumwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili wasije kusikiliza chochote katika wahyi au kinginecho, isipokuwa atakayeiba kusikiliza na akasalimika na kupigwa kimondo.
  • Majini hujifanyia vipenzi katika binadamu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)