Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 6045

Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لاَ يَرْمِي رَجُلٌ رَجُلًا بِالفُسُوقِ، وَلاَ يَرْمِيهِ بِالكُفْرِ، إِلَّا ارْتَدَّتْ عَلَيْهِ، إِنْ لَمْ يَكُنْ صَاحِبُهُ كَذَلِكَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Dharri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo".

English translation

Abu Dharr (may Allah be pleased with him) reported that he heard the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "No man accuses another man of defiant disobedience or accuses him of disbelief except that it rebounds on him if his companion is not like that."

Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema kumwambia mwingine: Wewe ni muovu, au: Wewe ni kafiri, ikiwa hatokuwa kama alivyosema, basi yeye ndiye atakayestahiki sifa iliyotajwa, na kauli yake itarudi kwake, na ama akiwa kama alivyosema basi hakuna kitakachorejea kwake; kwa sababu atakuwa mkweli katika hayo aliyoyasema.

Faida

  • Uharamu wa kuwatuhumu watu kwa ukafiri au uovu, pasina sababu ya kisheria.
  • Ulazima kupata uhakika katika utoaji wa hukumu kwa watu.
  • Amesema bin Daqiq Al-Iddi: Na hii ni tahadhari kubwa kwa atakayemkufurisha yeyote katika waislamu haliyakuwa hayuko hivyo, na huku ni kujitia mtegoni kukubwa.
  • Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Lakini haipelekei kutokuwa kwake muovu au kafiri kutokupata dhambi katika sura ya kauli yake: Wewe ni muovu, bali katika sura hii kuna mchanganuo: Ikiwa atakusudia kumnasihi au kumnasihi mtu mwingine kwa kubainisha hali yake hapa itafaa, na ikiwa atakusudia kumuaibisha na kumtangaza kwa hilo na kumuudhi haitafaa; kwa sababu ameamrishwa na sheria kumsitiri na kumueleimisha na kumpa mawaidha kwa njia nzuri, kwa namna yoyote itakayowezekana kwake kuitumia kwa upole basi haifai kwake kutumia ukali; kwa sababu inaweza kuwa sababu ya kumhadaa na kumfanya aendelee na hilo, kama ilivyo tabia ya baadhi ya watu pale upole usipotumika, na hasa hasa atapokuwa muamrishaji yuko chini ya muamriwa katika cheo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)