Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 243

Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قال: أَخْبَرَنِي عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: أَنَّ رَجُلًا تَوَضَّأَ فَتَرَكَ مَوْضِعَ ظُفُرٍ عَلَى قَدَمِهِ فَأَبْصَرَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «ارْجِعْ فَأَحْسِنْ وُضُوءَكَ» فَرَجَعَ، ثُمَّ صَلَّى.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Jabiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amenieleza Omari Bin Khattwab: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali.

English translation

Jābir (may Allah be pleased with him) reported: ‘Umar ibn al-Khattāb said to me: A man performed ablution and left a small part on his foot equal to the size of a nail unwashed. The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) saw that and said: "Go back and perform your ablution properly." He performed it again and prayed.

Maelezo

Ameeleza Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuona mtu mmoja kamaliza kutia udhu wake, akaacha kiasi cha kucha moja katika kisigino chake, hakikupatwa na maji ya udhu, akasema kumwambia huku akiashiria sehemu palipo na mapungufu: Rudi katie vizuri udhu wako, na utimize na ukipe kila kiungo haki yake katika maji, yule bwana akarudi akatimiza udhu wake kisha akaswali.

Faida

  • Uwajibu wa kufanya haraka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kumuelekeza asiyejua na aliyeghafilika, na hasa hasa uovu ukiwa unaambatana na kuharibika kwa ibada yake.
  • Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vya udhu, nakuwa mwenye kuacha sehemu ya kiungo -hata kama ni kidogo- udhu wake hautasihi, na itamlazimu kurudia ikiwa umepita muda mrefu tangu kumaliza udhu wake.
  • Sheria ya kupendezesha udhu, na hii ni kwa kuutimiza na kueneza vizuri kwa namna iliyoamrishwa kisheria.
  • Miguu miwili ni katika viungo vya udhu, na haitoshi kuifuta, bali ni lazima kuiosha.
  • Ni lazima kufuatanisha baina ya viungo vya udhu, kiasi kwamba aoshe kila kiungo kabla hakijakauka kilicho kabla yake.
  • Kutojua na kusahau havidondoshi wajibu, bali vinadondosha dhambi, huyu bwana ambaye hakutimiza udhu wake kwa sababu ya kutojua kwake, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakumdondoshea uwajibu, ambao ni udhu, bali alimuamrisha kurudia.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)