Nyuma

Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قال: أَخْبَرَنِي عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: أَنَّ رَجُلًا تَوَضَّأَ فَتَرَكَ مَوْضِعَ ظُفُرٍ عَلَى قَدَمِهِ فَأَبْصَرَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «ارْجِعْ فَأَحْسِنْ وُضُوءَكَ» فَرَجَعَ، ثُمَّ صَلَّى.

Kutoka kwa Jabiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amenieleza Omari Bin Khattwab: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali.

Jābir (may Allah be pleased with him) reported: ‘Umar ibn al-Khattāb said to me: A man performed ablution and left a small part on his foot equal to the size of a nail unwashed. The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) saw that and said: "Go back and perform your ablution properly." He performed it again and prayed.

Uwajibu wa kufanya haraka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kumuelekeza asiyejua na aliyeghafilika, na hasa hasa uovu ukiwa unaambatana na kuharibika kwa ibada yake.

Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vya udhu, nakuwa mwenye kuacha sehemu ya kiungo -hata kama ni kidogo- udhu wake hautasihi, na itamlazimu kurudia ikiwa umepita muda mrefu tangu kumaliza udhu wake.

Sheria ya kupendezesha udhu, na hii ni kwa kuutimiza na kueneza vizuri kwa namna iliyoamrishwa kisheria.

Miguu miwili ni katika viungo vya udhu, na haitoshi kuifuta, bali ni lazima kuiosha.

Ni lazima kufuatanisha baina ya viungo vya udhu, kiasi kwamba aoshe kila kiungo kabla hakijakauka kilicho kabla yake.

Kutojua na kusahau havidondoshi wajibu, bali vinadondosha dhambi, huyu bwana ambaye hakutimiza udhu wake kwa sababu ya kutojua kwake, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakumdondoshea uwajibu, ambao ni udhu, bali alimuamrisha kurudia.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 243 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:8386