Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «إِنَّ لِلْمُؤْمِنِ فِي الْجَنَّةِ لَخَيْمَةً مِنْ لُؤْلُؤَةٍ وَاحِدَةٍ مُجَوَّفَةٍ، طُولُهَا سِتُّونَ مِيلًا، لِلْمُؤْمِنِ فِيهَا أَهْلُونَ، يَطُوفُ عَلَيْهِمِ الْمُؤْمِنُ فَلَا يَرَى بَعْضُهُمْ بَعْضًا».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abuu Musa radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake, amesema: "Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao".
English translation
Abu Mūsa (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Verily, the believer in Paradise will have a tent made of a single hollow pearl, the length of which is sixty miles. The believer will have wives therein whom he will visit in turn, and they will not see each other."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya neema za peponi, nakwamba muumini ndani ya pepo atakuwa na hema pana kwa ndani, lilitokana na madini ya lulu yenye kung'aa, upana wake na urefu wake kuelekea juu ni maili sitini, katika kila mahali na kila kona katika kona zake nne kuna wake, na wote hawaonani, muumini atakuwa akiwazungukia.
Faida
- Kumebainishwa ukubwa wa neema za watu wa peponi.
- Himizo la kufanya amali njema kwa kubainishwa yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu kwa ajili yao miongoni mwa neema.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.