Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ أَدْنَى مَقْعَدِ أَحَدِكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ أَنْ يَقُولَ لَهُ: تَمَنَّ فَيَتَمَنَّى، وَيَتَمَنَّى، فَيَقُولُ لَهُ: هَلْ تَمَنَّيْتَ؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ، فَيَقُولُ لَهُ: فَإِنَّ لَكَ مَا تَمَنَّيْتَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika, mwenye kiwango cha chini zaidi kati yenu katika Pepo ni kwamba ataambiwa: "Tamani!" Basi atatamani na atamani, na ataambiwa: "Je umeshatamani?" Atasema: "Nidyo." Ataambiwa: "Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo."
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Indeed, the lowest position of one of you in Paradise is that He will say to him: Wish, and he will wish and wish. Then He will say to him: Did you wish? And he will say: Yes. Then He will say to him: For you is what you wished, and the like of it along with it."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye nafasi na daraja ndogo zaidi kwa wale watakaoingia peponi, ataambiwa: Tamani, basi atatamani, na atatamani tena, mpaka atafikia mahali ataishiwa yote ya kutamani isipokuwa atayataja, hapo ataambiwa: Je, umetamani umefika mwisho? Atasema: Ndiyo, hapo ataambiwa: Basi ni vyako vyote ulivyotamani na mfano wake pamoja navyo.
Faida
- Kutofautiana kwa nafasi za watu wa peponi.
- Kumebainishwa ukubwa wa karama ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Neema za peponi hazishii katika kitu maalumu, bali muumini atapata ndani yake kila anachokitamani na nafsi yake kuwa na hamu nacho, ikiwa ni fadhila na ukwasi na ukarimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.