“Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى لِأَهْوَنِ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا يَوْمَ القِيَامَةِ: لَوْ أَنَّ لَكَ مَا فِي الأَرْضِ مِنْ شَيْءٍ أَكُنْتَ تَفْتَدِي بِهِ؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ، فَيَقُولُ: أَرَدْتُ مِنْكَ أَهْوَنَ مِنْ هَذَا، وَأَنْتَ فِي صُلْبِ آدَمَ: أَلّاَ تُشْرِكَ بِي شَيْئًا، فَأَبَيْتَ إِلَّا أَنْ تُشْرِكَ بِي».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio, atasema: Nilikutakeni jambo jepesi zaidi kuliko hili, nanyi mkiwa katika mgongo wa Adam: yakuwa msinishirikishe na chochote, mkakataa isipokuwa kunishirikisha na chochote".
English translation
Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Allah Almighty will say to the one receiving the least torment in Hellfire: 'If everything on earth was yours, would you ransom yourself with it?' He will say: 'Yes.' He will say: 'I had asked you for something easier than that when you were in the backbone of Adam: not to associate partners with Me, but you insisted on associating partners with Me.'"
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu ambao watateswa kidogo na Moto wa Jahannam baada ya kuingia humo: Lau mngekuwa na dunia na vyote vilivyomo ndani yake, mngeweza kujikomboa kutokana na mateso haya? Watasema: Ndio, Basi Mwenyezi Mungu atasema: Nilikutaka na nikakuamrisheni jambo jepesi kuliko hilo, ilipo chukuliwa ahadi kwenu mkiwa katika mgongo wa Adam, ya kwamba msinishirikishe na chochote. Nilipowatoa katika dunia hii mlikataa kufanya chochote isipokuwa ushirikina.
Faida
- Thamani ya tauhidi na wepesi wa kuifanyia kazi.
- Hatari ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu kingine na mwisho wake mbaya.
- Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kwa wanadam wote wakiwa katika mgongo wa baba yao Adam ya kutomshirikisha.
- Tahadhari ya ushirikina nakuwa thamani ya dunia yote haiwezi kumsaidia chochote kafiri siku ya Kiyama.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.