Hakuna haki yoyote ya mtu muislamu anayotakiwa kuitolea usia, isipokuwa ahakikishae halali siku tatu, isipokuwa usia wake uwe umeandikwa kwake
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهُما أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا حَقُّ امْرِئٍ مُسْلِمٍ لَهُ شَيْءٌ يُوصِي فِيهِ، يَبِيتُ ثَلَاثَ لَيَالٍ، إِلَّا وَوَصِيَّتُهُ عِنْدَهُ مَكْتُوبَةٌ»، قَالَ عَبْدُ اللهِ بْنُ عُمَرَ رضي الله عنهما: «مَا مَرَّتْ عَلَيَّ لَيْلَةٌ مُنْذُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ذَلِكَ إِلَّا وَعِنْدِي وَصِيَّتِي».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakuna haki yoyote ya mtu muislamu anayotakiwa kuitolea usia, isipokuwa ahakikishae halali siku tatu, isipokuwa usia wake uwe umeandikwa kwake", akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: "Haukuwahi kupita usiku mmoja tangu nilipomsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa usia wangu nilikuwa nao".
English translation
Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported that he heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "It is not proper for a Muslim who has something to bequeath to stay for three nights without having his will written with him." ‘Abdullah ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) said: "Since I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say this, not a single night has passed without my will being with me."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa haitakiwi kwa muislamu anapokuwa na kitu cha kutolea usia katika haki au mali hata kama ni ndogo, alale siku tatu, isipokuwa ahakikishe usia wake umeandikwa kwake. Akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Sikuwahi kulala hata usiku mmoja tangu nilipomsikia rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa nilikuwa nikikaa na usia wangu.
Faida
- Sheria ya kuandika usia na kuharakisha kulifanya hilo, kwa kulibainisha, na kutekeleza amri ya sheria ndani yake, na kujiandaa na kifo, na kuuonyesha na mahali pa kuutekeleza, kabla mtu hajashughulishwa na lenye kumshughulisha.
- Usia: Maana yake ni ahadi, nayo ni mtu kumuahidi mtu mwingine baada ya kifo chake kupewa chochote katika mali yake, au akamuahidi mtu kumlelea watoto wake wadogo, au akamuahidi mtu katika kitu chochote katika matendo anayoyamiliki, baada ya kifo chake.
- Usia unagawanyika sehemu tatu: 1- Wa Sunna, nao ni usia wa mtu katika baadhi ya mali yake, itumike katika njia za kheri, na hisani; ili zimfikie thawabu zake baada ya kifo chake. 2- Usia wa wajibu, nao ni usia wa mtu kwa haki zilizo juu yake, sawa sawa haki hizo ziwe ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama zaka ambayo hakuitoa, au kafara, na mfano wake katika yale ya wajibu kwake katika msingi wa sheria, au haki hizi zikawa ni za wanadamu; kama deni, na kutekeleza amana. 3- Na Usia wa haramu: Nao ni pale atakapozidisha katika usia wake zaidi ya theluthi ya mali yake, au atakapotoa usia kwa mtu mwenye haki ya kumrithi.
- Ubora wa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao, na kwenda kwake haraka kufanya mambo ya kheri, na kufuata sheria tukufu.
- Amesema bin Daqiq Al-Idd: Na kuruhusu kukaa siku mbili mpaka tatu ni kwa sababu ya kuondoa uzito na ugumu.
- Na mambo muhimu ni lazima yadhibitiwe kwa maandishi; kwa sababu hilo huthibitisha na kuhifadhi haki zaidi.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.