Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قالَ: قالَ رَسُولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْه وسلَّمَ: «دِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ فِي سَبِيلِ اللهِ، وَدِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ فِي رَقَبَةٍ، وَدِينَارٌ تَصَدَّقْتَ بِهِ عَلَى مِسْكِينٍ، وَدِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ عَلَى أَهْلِكَ أَعْظَمُهَا أَجْرًا الَّذِي أَنْفَقْتَهُ عَلَى أَهْلِكَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako".
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "A dinar you spent in the cause of Allah, a dinar you spent on a slave, a dinar you gave in charity to a needy person, and a dinar you spent on your family; the greatest in reward is the one you spent on your family."
Maelezo
Ametaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya aina za utoaji, akasema: Dinari uliyoitoa katika Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari uliyoitoa katika shingo ya mtumwa, na dinari uliyoitoa sadaka kwa masikini mwenye uhitaji, na dinari uliyoitoa kwa watu wako na familia yako, kisha akaeleza kuwa yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni ile uliyoitoa kwa watu wako na familia na wale wanaokulazimu kuwahudumia.
Faida
- Wingi wa milango ya kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
- Kutanguliza kilicho bora katika mlango wa kutoa panapokuwa na msongamano wa mambo, na miongoni mwake ni kutoa kwa familia uwezo unapokosekana wa kuyatekeleza yote.
- Amesema Nawawi katika kitabu cha Sharhe Muslim: Himizo la kutoa matumizi kwa familia, na kumebainishwa ukubwa wa thawabu ndani yake; kwa sababu wako miongoni mwao wanaomlazimu kuwahudumia kwa sababu ya ukaribu wa udugu, na yuko miongoni mwao inakuwa ni sunna na inakuwa ni sadaka na kuunga udugu, na yuko ambaye inakuwa wajibu kwa kummiliki kwa sababu ya ndoa au umiliki wa kuume (kama mateka na vijakazi), na hii yote ni fadhila iliyohimizwa, nayo ni bora kuliko sadaka ya hiyari.
- Amesema As-Sanadi: Kauli yake "Dinari anayoitoa kwa familia yake", Yaani: Atakaponuia kupata radhi za Allah na akakusudia kutoa katika familia kwa mfano haki.
- Amesema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo makubwa kuliko mtu anayetoa matumizi kwa familia ndogo anayowasitiri au Mwenyezi Mungu anawanufaisha kwayo na kuwatosheleza?!
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.