Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-5799

Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن عائشة رضي الله عنها قالت: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إنَّ المُؤْمِنَ ليُدرِكُ بِحُسْنِ خُلُقِهِ دَرَجَةَ الصَّائِمِ القَائِمِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku".

English translation

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "Verily, a believer can attain, by his good manners, the rank of one who fasts and prays often."

Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tabia njema humfikisha mwenye tabia hiyo nafasi ya mwenye kufunga mchana daima na kusimama usiku, na tabia njema inakusanywa na: Kutenda wema, na kauli nzuri, na uso mkunjufu, na kuacha maudhi na kuyavumilia kutoka kwa watu.

Faida

  • Uislamu umetilia umuhimu mkubwa kurekebisha tabia na ukamilifu wake.
  • Ubora wa tabia njema, mpaka mja humfikisha daraja ya mfungaji asiyefungua na mwenye kusimama usiku asiyechoka.
  • Kufunga mchana na kusimama usiku ni amali mbili kubwa, kuna uzito mkubwa sana kwa nafsi, lakini daraja yake ameifikia mwenye tabia njema kwa kupambana na nafsi yake ili kuwa na muamala mzuri na watu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)